Wednesday, 6 July 2016

WEMA SEPETU AFUNGUKA

BAADA YA DIAMOND KUMPOST WEMA SEPETU INSTAGRAM, WEMA AFUNGUKA JUU YA HILO KIUNAGA UBAGA.


Jana Nasibu Abdul maarufu Diamond Platnumz alipost picha ya Wema Sepetu katika ukurasa wake wa Instagram akiwataka watu wajitokeze kumsupport katika tamasha. Pamoja na Wema Sepetu, Diamond alimpost pia Idris Sultan na Christian Bella.
Bonyeza hapa  kwa taarifa kamili kuhusu habari hiyo.

Wema Sepetu alipohojiwa kuhusu kitendo hicho alisema kuwa amefurahi sana na kuona kama kuna mzigo alioutua kwani watu walikuwa wakitumia tofauti zao za kutengenezwa kama faida kwao ili kupata wafuasi (Followers).
Aidha, ameeleza kuwa yeye ni shabiki wa Diamond Platnumz na amekuwa akisikiliza nyimbo zake hata baada ya wao kuachana. Amesema kuachana kwao hakumfanyi asiwe shabiki wake.
Alieleza kuwa kwa muda sasa amekuwa akijizuia kuimba nyimbo za Diamond akiwa kwenye public lakini ameona kuwa anajikomoa yeye mwenyewe kwani akirudi kwenye gari lake huwa anaimba. Kwake amesema kuwa kitendo hicho kinaondoa uongo uliokuwa unasemwa kwamba wawili hao wana bifu zito.

No comments:

Post a Comment