PICHA YA RAIS JACOB ZUMA WA AFRIKA KUSINI AKIMBUSU MSICHANA YAZUA UTATA
Picha inayoaminika kuwa ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini akumbusu msichana anayeelezwa kuwa na umri wa miaka 19, imezua gumzo nchini Afrika Kusini.
Msichana huyo aliweka picha hii katika mtandao wa Facebook na kuandika “he is not just a blesser, we are deeply inlove and am greatful for all that he has done for me, much love. Xo xo.”
Raia wengine wa Afrika Kusini wanaeleza kuwa hawakushtushwa na picha hiyo kwani walidai Rais huyo ni mtu anayependa sana mambo hayo hivyo siyo jambo geni sana kwao.
Baada ya muda mfupi picha hiyo kuwekwa, akaunti ya msichana huyo haikuonekana tena na wengi wakiamini kuwa iliondolewa kwa agizo la Rais Zuma.
Rais Zuma alipotafutwa kuzungumza kuhusu hili alijibu kuwa “we will check the matter.”
No comments:
Post a Comment