Wednesday 6 July 2016

D'BANJ AFUNGA PINGU ZA MAISHA

D'BANJ MWANAMZIKI WA NIGERIA AFUNGA PINGU ZA MAISHA
Mwanamuziki kutoka Nigeria maarufu kama D’banj ameshangaza wengi baada ya taarifa za yeye kufunga pingu za maisha weekend iliyopita kusambaa.
Watu walishangaa kuona picha aliyopost kwenye mitandao ya jamii mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa amevaa pete na badae kukanushwa na kusema ile ilikua ni pete ya fasheni tu.
 Inasemekana kwamba D’banj amefunga ndoa na mtangazaji wa MTV katika kipindi cha Lip Sync Battle Didi Kilgrow, Jumamosi iliyopita kwenye sherehe ya kuzaliwa Baba wa mwanamuziki huyo.

Mpaka leo ‘The Kokomaster’ ambalo ni jina lingine la D’banj hajatoa statement yoyote kuhusu tetesi hizo, lakini Pongezi za kufunga ndoa bado zinaendelea kutoka kwa mashabiki wake.






No comments:

Post a Comment