HII NDIYO SABABU YA MKUU WA WILAYA MTEULE WA MBOZI KUIKATAA NAFASI HIYO?
Mkuu wa Wilaya (DC) Mteule wa Mbozi, Ally Masoud Maswanya ajiondoa katika nafasi hiyo ya ukuu wa wilaya na badala yake, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kongwa, John Ernest Palingo anakwenda kuwa DC Mbozi, na Kongwa itasubiri uteuzi mpya.
Kutoka kwenye mitandao ya kijamii, inadaiwa kuwa Ally Masoud Maswanya ambaye ni Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa mshahara wake anapokea baada ya makato yote ni milioni 20 hapo ikiwa bado hajapewa nyongeza (bonus) na marupu rupu mengine. Aidha inadaiwa kuwa kila baada ya miezi mitatu anapewa bonus ya kati ya shilingi milioni 10-15.
Watu wamedai kuwa hii ndio huenda ikawa na sababu ya Masoud kuubwaga ukuu wa wilaya. Inaelezwa kuwa maslahi anayayoyapata akiwa Tigo hawezi kuyapata akiwa serikali na pia ukichangia serikali ya awamu yatano ni Hapa Kazi Tu, basi kibarua chako kinakuwa hatarini muda wote
No comments:
Post a Comment