Saturday, 16 July 2016

UKIUKWAJI WA MAADILI


BASATA YAUFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO


Baraza ka Sanaa nchini (BASATA) limeufungia wimbo wa mwanamuziki Nay wa Mitego unaokwenda kwa jina la Pale kati Patamu kwa maelezo kuwa wimbo huo kwa kiasi kikubwa umekiuka maadili ya sanaa na jamii kwa ujumla.
Nay wa Mitego imeelezwa kuwa amekuwa akitoa nyimbo na kufanya matamasha ya muziki ambayo si kwamba ni kinyume na maadili ya Tanzania lakini pia amekuwa akiwadhailisha wanawake kwa picha anazopiga na maneno anayoyaumia katika nyimbo zake.
Nay wa Mitego hivi karibuni emetoa wimbo wake wa Pale Katipatamu ambao picha za wimbo huu zimesambaa mitandaoni zikionyesha wasichana waliopiga picha wakiwa utupu kitu ambacho si sawa.
BASATA limewakumbusha wasanii woe nchini kufanya kazi kufuatana na taratibu zilizopo lakini pia kuangalia maadali ya nchi ili kuhakikisha kuwa mikwaruzano isiyokuwa yalazima inaepukika na kunakua na ushirikiano wa kuinua tasnia nzima ya sanaa nchini.


















No comments:

Post a Comment