Wednesday, 6 July 2016

ABIRIA ASAHAU MA MILLIONI YA HELA KWENYE TAXI

ABIRIA ASAHAU SHILINGI MILIONI 375 KWENYE TAXI, SOMA ALICHOKIFANYA DEREVA TAXI.



Je! Mtu akisahau kitita cha fedha nyumbani au kwenye gari lako utafanyaje? Soma kisa cha dereva taxi huyu.
Dereva taxi mmoja nchini Marekani, Raymond MacCausland maarufu “Buzzy,”siku ya Jumamosi alikumbana na bahati kubwa baada ya kukuta fedha nyingi kwenye siti ya nyuma ya gari lake baada ya abiria aliyekuwepo kuzisahau.Dereva huyo alikuta abiria wake aliyempeleka eneo la Boston USA, alisahau $187,000 (TZS milioni 375). Kilichowashangaza wengi ni uamuzi aliouchukua dereva huyo mara alipoona fedha hizo.

Buzzy aliamua kuzipeleka fedha hizo katika kituo cha Polisi Boston na Polisi walisema kuwa fedha hizo ni mali ya mwanaume mmoja ambaye amezipata baada ya kuuza mali za urithi.
Dereva huyo alipohojiwa kuhusu uamuzi wake huo alisema kuwa hivyo ndivyo alivyolelewa kuwa mwaminifu na ametenda kama alivyopaswa kutenda. Aidha, amesema kuwa alizikuta fedha hizo alipokuwa akitafuta baadhi ya vitambulisho kwenye gari lake.Mwenye fedha hizo alimpatia dereva huyo kiasi cha USD 100 kama shukrani kwa uaminifu wake.



No comments:

Post a Comment