Saturday 16 July 2016

WATUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA WAJISALIMISHA

WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA 60,000 WAJISALIMISHA BAADA YA RAIS KUAGIZA WAUAWE POPOTE WALIPO


Takribani watumiaji wa dawa za kulevya 60,000 wamejisalimisha kwenye mamalaka husika baada ya Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino kuwaambia wananchi wawaue popote pale watakapowaona.


Rais huyo ambaye alishinda uchaguzi wa Mei mwaka huu, aliahidi kupammbana na dawa za kulevya ndani ya nchi hiyo. Alisema kuwa wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya wamekuwa wakiwaharibu watu wengine ambao hawatumii.


Jeshi la Polisi nchini humo limeeleza kuwa watu 110 wanaohusishwa na dawa za kulevya wameshauawa tangu Rais huyo alipoingia madarakani lakini vyombo vya habari vya ndani vimesema kuwa idadi ya waliouawa wanakaribia 200.


Rais Rodrigo ameonya huenda damu zaidi ikamwagika ikiwa ni njia ya kuhakikisha kuwa habari za dawa za kulevya zinakwisha. Ameahidi kuwalinda Polisi dhidi ya sheria pale watakapomuua polisi.





No comments:

Post a Comment