sababu ya BAADHI YA WA-AFRIKA WANAREJEA NYUMBANI KUTOKA UGHAIBUNI.
atu wengi sana kutoka barani Afrika wamekuwa wakizunguka katika nchi nyingi na mabara tofauti lakini mara zote, Ulaya na Amerika ya Kaskazini ni maeneo mawili ambapo wa-Afrika wengi wamevutiwa kwenda kuishi ambapo takribani wahamiaji milioni 8.8 wanaishi katika maeneo hayo mawili.
Kuanzia mwaka jana, kumekuwa na ongezeko kubwa la watu kukata tiketi za moja kwa moja za kurudi makwao na kuiaga Marekani, Canada na bara Ulaya.
Waafrika wengi waliopo nchi za magharibi wanasoma au wanafanyakazi huku wakifurahia maisha mazuri ya huko,. Lakini bado wamekuwa ni nguzo muhimu ya uchumi wa Afrika kwani kwa mwaka 2012 inaelezwa kuwa kiasi cha fedha dola bilioni 64.3 zilitumwa na wa-Afrika waishio nje.
Kupata visa ya kusafiria si kazi ndogo, ndio maana inashangaza sana kuona raia kutoka Afrika waliopo nje ya nchi wakikubali kwa maamuzi yao wenyewe kurejea makwao. Lakini ukweli ni kuwa kuna sababu kwanini wanakubali kurudi makwao.
Baadhi ya wanaorejea Afrika wameeleza kuwa wanarudi kutokana na fursa zilizopo katika mataifa mengi ya Afrika yanayokua kiuchumi na kuwa wanaamini uzoefu na ujuzi walioupata kutoka ughaibuni utawasaidia kuchangia maendeleo ya nchi zao.
Wengine wamenukuliwa wakisema kuwa wanarejea Afrika kwa sababu ya uzalendo. Kama kundi lililopita walivyoeleza, hawa nao wanaamini wana wajibu wa kuitumikia jamii yao baaada ya kupata ujuzi kutoka katika nchi za magharibi. Baadhi ya hawa ni madaktari, maprofesa.
Kundi jingine lilieleza kuwa wao wanarudi nyumbani (Afrika) kwa sababu ya wale waliowaacha nyuma wakati wakienda ughaibuni. Walisema kuwa waliwakumbuka ndugu, jamaa na marafiki zao na kuona kuwa familia yao kubwa iko Afrika hivyo waliamka siku na kuona bora wabebe vyao na kurudi kuungana na familia zao.
Inaelezwa kuwa wengi wanaporejea kutoka ughaibuni wanapata changamoto nyingi sana ikiwa na pamoja na watu kuamini kuwa ukitoka ughaiuni basi utakuwa na fedha nyingi sana za kumpa kila mmoja. Lakini wengine wamekumbana na changamoto katika utendaji wa serikali. Hawa wamesema kuwa serikali za magharibi zipo makini na kuwa inawawia vigumu wao kuishi Afrika ambapo serikali hazipo makini na wakati mwingine huamua kurudi ughaibuni.
No comments:
Post a Comment