Saturday 16 July 2016

JARIBIO LA MAPINDUZI YA KIJESHI SERIKALI YA UTURUKI

WATU 66 WAUAWA, MAMIA WASHIKILIWA KATIKA JARIBIO LA KUPINDUA SERIKALI UTURUKI


Takaribani watu 60 wameuawa nchini Uturuki huku wengine 336 wakishikiliwa na Jeshi la nchini hiyo kufuatia tukio la usiku wa kuamkia leo Julai 16 ambapo kulikkuwa na jaribio la kutaka kupindua serikali ya nchi hiyo.


Usiku wa kuamkia Julai 16 kwa saa za Afrika Mashariki, kikundi cha Wananjeshi wa Uturuki kilitangaza kupitia televisheni kuwa wamepindua serikali ya nchi hiyo na kuwa wao ndio wapo madarakani.
Muda mfupi baadae Waziri Mkuu wa nchi hiyo alizungumza na kusema kuwa, serikali hiyo iliyokuachaguliwa na watu itaendelea kuwa madarakani hadi pale wananchi walioichagua kuamua kuwa sasa iondoke na si vinginevyo.

Wakati wa tukio hilo, mitandao ya kijamii ilifungwa, viwanja vya ndege vilfungwa na nchi kuwekwa chini ya ulinzi mkali. Katika hatua nyingine, Mku wa Jeshi la Uturuki alikuwa akishikiliwa na kikundi kilichojaribi kupindua serikali.
Rais wa Uturuki,  Recep Tayyip Erdoğan ametangaza na kusema kuwa jaribio la kupindua serikali limeshindwa na sasa mambo ni shwari.



No comments:

Post a Comment