Monday, 20 June 2016

SHILOLE AZIDI KULIA NA WASANII WENZAKE

DAR ES SALAAM: Msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameonesha masikitiko yake kufuatia madai ya kudhalilishwa na baadhi ya wasanii wenzake kwa kuipa promo video ya wimbo mpya wa zilipendwa wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ wa Jike Shupa.

Kwa mujibu wa Shilole, video ya wimbo huo inaonesha matukio ya kumdhalilisha ambayo inaonekana yeye alikuwa akimfanyia Nuh enzi za uhusiano wao kama vile kumpiga na kumzodoa, mambo ambayo hakuwahi kuyafanya.

“Nimesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya wasanii wenzangu kuiposti video hiyo kwenye mitandao mbalimbali, huko ni kunidhalilisha kwa sababu jamii ikiangalia inaweza kunitafsiri tofauti,” alisema Shilole.

Katika video hiyo, msichana anayefanana na Shilole aitwaye Zuwena aliyetumika kama video queen anaonekana akimfanyia vitimbi Nuh huku akitafsiriwa kuwa, ndivyo Shilole alivyokuwa akimfanyia jamaa huyo.

NA IMELDA MTEMA, Ijumaa
KTK - Global Publishers

No comments:

Post a Comment