Baada ya mwanadada Linah Sanga kusema anatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama za Darassa, rapa huyo wa wimbo ‘Kama Utanipenda’ amefunguka na kuzungumzia kauli hiyo.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Darassa amesema anaheshimu mawazo ya mwanadada huyo.
“Hiyo ni kauli yake, naheshimu mawazo yake. Nimefunzwa kuheshimu maoni ya kila mtu, kwa hiyo sina la kuzungumza zaidi ya hapo kwa sababu hizo ni issue za privacy za watu,” alisema Darassa.
Katika hatua nyingine Darassa amewataka mashabiki wake wa muziki kukaa mkao wa kula wa ujio wa kazi yake mpya ambayo ataiachia katikati ya mwezi huu.
No comments:
Post a Comment